MAMBO 10 MUHIMU YANAYOATHIRI UANGUAJI WA MAYAI YA KUKU.
1. UBORA WA CHAKULA.
Chakula cha kuku hutakiwa kuwa kikamilifu na chenye vitamini na madini ya ziada kwani tofauti baina ya chakula cha kuku wa mayai na kuku wazazi nk wingi wa vitamini na madini.
Unashauriwa kutumia premix ya ANUPCO BREEDERS PREMIX kiasi cha 2.5kg kwa tani moja au GLP 1Kg kwa kila kilo 50 ya chakula.
Chakula kiwe bora na chenye kutosha, upungufu wa calcium husababisha mayai kuwa hayafai kwa kuzalishia, pia upungufu wa chumvi husababisha kuku kudonoana manyoya na kulana nyama, chumvi hutakiwa kuwa asilimia 4% ya chakula chote.
2. UFUGAJI MZURI WA KUKU WAZAZI.
Maji yawe ya kutosha na safi na salama. Upungufu wa maji ya husababisha upungufu wa wingi wa mayai na pia upungufu wa ubora wa mayai.
A. Kuku wazazi wapewe chanjo zote muhimu.
B. Hali ya joto katika banda la kuku pia kuathiri uzalishaji.
C. Hali ya joto Kali katika banda la kuku inaathiri moja kwa moja uzalishaji wa mbegu katika madume kwa hiyo husababisha mayai yasiwe na mbegu.
3. UWIANO WA MADUME NA. MAJIKE.
Unatakiwa uwe na jogoo moja kwa matetea saba hadi nane wa kienyeji ndipo jogoo ataweza kuyahudumia vizuri na kuweza kutotolesha mayai yenye mbegu pia.
4. MAZINGIRA
Mazingira mazuri ya kiatamio (incubator) bora. Kuku wawekewe mazingira mazuri yasiyo na upepo mkali, joto kali, baridi kali, viroboto, panya, paka na pawe na matandiko. Kiatamio bora unashauriwa kutumia vitamini vya VETKING vinavyopatikana Farmers. Centre na farmbase hapa nchini tanzania.
5. UBORA WA MAYAI YA KUZALISHIA.
Mayai yawe safi, yasioshwe, yawe na ukubwa wa wastani sio makubwa sana wala si madogo sana na umbile la kawaida. Sio la viini viwili na lisiwe na ufa.
6. HIFADHI BORA YA MAYAI.
Baada ya kutagwa mayai yahifadhiwe katika hali ya ubaridi wa 0.6°C hadi 2.2°C na yasizidi muda wa siku 10 hadi 14 kabla ya kuwekwa kwenye incubator baada ya siku hiyo uwezo wa yai kuanguliwa huwa mdogo sana.
7. HALI YA JOTO Katika kiatamio inatakiwa uwe 37-38 wakati wote wa kuatamia. Ujoto huo ukipungua chini ya 35.6 au kuzidi juu ya 39.4% vifo huweza kutokea.
8. KIATAMIO kinapogeuza mayai kinaiga mwendo halisi wa kazi ya kugeuza mayai inavyoyafanya na kuku muatamiaji. Kama kiatamio hakijiendeshi chenyewe ni jukumu lako wewe mfugaji kuyageuza mayai walau mara tano kwa siku.
9. UNYEVUNYEVU
Hali ya joto katika kuzalisha mayai ni muhimu sana kuangulia vifaranga kwa makini
Hali hiyo ( humidity) huathiri upoteaji wa maji ya madini ya yai na kusababisha vifo vya vifaranga ndani ya yai au uzito wa vifaranga baada ya kuzaliwa. Kuwa makini sana na kiasi cha maji kinachotakiwa kiwepo katika incubator wakati wote.
10. Uwekaji wa mayai katika hali ya ubaridi uwe ncha juu na tumbo chini kwembamba juu na kunene chini. Mayai yanapohifadhiwa ncha juu yana nafasi kubwa ya kuangua kuliko yanayowekwa tumbo juu.
No comments:
Post a Comment